Simamia shule yako
bila makaratasi.

Matokeo, ada, mahudhurio na mawasiliano na wazazi — vyote mahali pamoja. Umejengwa kwa ajili ya shule za Tanzania, unaendana na viwango vya NECTA.

NECTA grading Wazazi wanaona matokeo kwa simu Hakuna server ya kununua
Vipengele

Kila kitu shule inachohitaji

Kuanzia kuandika alama hadi mzazi kupokea matokeo — mfumo mmoja unaofanya kazi pamoja.

Matokeo

Walimu wanaandika alama, mfumo unahesabu daraja na division. Mkuu anaidhinisha kabla hayajatolewa.

Ada na Malipo

Weka ada kwa darasa na muhula, rekodi malipo, salio linahesabiwa lenyewe. Matokeo yanafungwa hadi ada ilipwe.

Mahudhurio

Andika mahudhurio ya kila siku kwa dakika moja. Ripoti ya kila mwanafunzi na muhtasari wa darasa.

Mzazi kwenye Simu

Wazazi wanaingia na kuona matokeo, ada na mahudhurio ya watoto wao — muda wowote.

Matangazo

Tuma ujumbe kwa wazazi wote au darasa moja. Kila mtu anapata taarifa kwa wakati.

Ripoti

Ripoti za ada, ufaulu na mahudhurio — zionekane, zipakuliwe PDF au Excel.

Jinsi Inavyofanya

Kuanza ni rahisi

Tunasajili shule yako

Tunaweka madarasa, masomo, walimu na wanafunzi. Unaweza kuleta orodha kwa Excel.

Wafanyakazi wanafunzwa

Mafunzo ya saa mbili yanatosha. Kila mtu anaona tu kazi yake — hakuna mkanganyiko.

Mnaanza kutumia

Alama, ada na mahudhurio vinaingia kwenye mfumo. Wazazi wanaanza kuona matokeo.

Wasiliana Nasi

Omba bei na demo

Tuambie kuhusu shule yako, tutakupigia na kukuonyesha mfumo bila malipo.